
Enedy Mwanakatwe Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Geita
Hayo yamesemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, yenye kauli mbiu ya "Kila uhai una thamani", huku baadhi ya wanaume wakielezea sababu za wao kutopata sauti zao.
"Matukio ya ukatili yaliyotolewa taarifa ni 26, katika natukio hayo, ubakaji yamekuwa ni saba, ulawiti wawili na vipigo ni 17, pamoja na matukio hayo kutolewa taarifa na wanawake na watoto, lakini pia wanaume baadhi wamekuwa ni wahanga wa ukatili japokuwa hawatoi taarifa katika ofisi zetu na hivyo kukosa takwimu zao kwa urahisi", amesema Mwanakatwe.
Kwa upande wake mwananchi wa mkoa huo amesema, "Sisi kama wanaume tunafanyiwa sana ukatili wa kijinsia na wanawake yani wake zetu lakini unashindwa kuanzia kwamba uende wapi kwa sababu sisi huwaga hawatujali sana, mnaowajali sana ni wanawake, sasa ninashindwa kuelewa labda kwa siku ya leo kwa kuwa waandishi mmekuja mimi lazima nitoe tu ya ukweli hata sisi tunateswa sana", alisema Mashiri.
Msimamizi wa maswala ya kijinsia kutoka shirika la Plan International Hildegada Mashauri amewaomba wananchi kutoa taarifa za ukatili ili jamii itakapoona watuhumiwa wamechukuliwa hatua itapunguza vitendo hivyo.
Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo, amewataka wananchi na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoishia kwenye siku16 za kupinga ukatili badala yake wafanye kama mtindo wao wa maisha ili kuepusha vitendo vya ukatili vilivyokithiri wilayani humo.