
Mabingwa watetezi wa Kombe hilo, klabu ya Yanga itaanza kampeni ya kutetea Ubingwa wao kwa kucheza dhidi ya Kurugenzi FC ya mkoani Simiyu kwenye dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam huku makamu bingwa Coastal Union wamepangwa kucheza na Tanga Middle jijini Tanga.
Simba SC wamepangwa kucheza dhidi ya Eagle FC ya jijini Dar es Salaam kwenye dimba la Mkapa jijini humo ilhali waoka mikate klabu ya Azam ikitaraji kucheza dhidi ya Malimao FC ya mkoani Katavi.
Mara baada ya droo hiyo kukamilika, meneja wa mashindano hayo Baraka Kizuguto ametoa rai kwa timu zote kujiandaa vema kwani shindano hilo ndilo linalotoa mwakilishi wa kwenda kushiriki kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Ratiba nzima ilivyo
Geita Gold vs Transit Camp (Nyankumbu, Geita)
Ihefu vs Mtama Boy (Highland State)
Kagera Sugar vs Buhare FC (Kaitaba)
Dodoma Jiji vs TMA Stars (Jamhuri,Dodoma)
Ruvu Shooting vs Ndanda (Uhuru)
Namungo vs Kitayosce (Majaliwa)
Polisi Tz vs Nyika FC (Ushirika)
Mbeya City vs Stand Fc (Sokoine)
Mtibwa Sugar vs TRA (Manungu)
Prisons vs Misitu (Sokoine)
Singida Bs vs Lipuli Fc (Liti)
Coastal Union vs Tanga Middle (Mkwakwani)
KMC VS Tunduru (Uhuru)
Azam vs Malimao (Chamazi)
Fountain Gate vs Rhino Rangers (Jamhuri, Dodoma)
JKT Tanzania vs Biashara Utd (Mej G. Isamuhyo)