Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Washindwa kusali baada ya kanisa kubadilishwa jina

Monday , 5th Dec , 2022

Waumini wa kanisa la EAGT jimbo la Mwanza kusini wamekumbwa na taharuki baada ya kukuta kanisa lao limebadilishwa jina bila wao kujua hali iliyozua mzozo katika kanisa hilo na kusababisha shughuli zote za ibada kukwama

Wakizungumza na EATV viongozi wa kanisa hilo wamesema mgogoro huo uliibuka siku nne zilizopita lakini ghafla wakashangaa Jumapili wakakuta jina la kanisa hilo limebadilishwa na kuandikwa ASSEMBLIES OF GOD GOSPEL CHURCH INTERNATIONAL AGGCI na wakishindwa kuelewa nini kimetokea huku umiliki wa eneo hilo ukisoma kwa jina la kanisa la EAGT

Mchungaji Boaz Kazeba ndiye anadaiwa kubadilisha kanisa hilo la EAGT na kuwa AGGCI lililopo eneo la Bugarika mtaa wa Zahanati kata ya Pamba jijini Mwanza

"Sikutaka nifanye kitu chochote kile lakini umesikia wameniita mimi gaidi sijui muhuni, elishababu sijui nashangaa na huyo aliyesema mimi ni muumini wangu wa zamani anayosema ametoa kiwanja ana vielelezo? Hapa sisi tulimjengea mtu nyumba ya vyumba vitatu na maandishi ninayo siyo kama nazungumza kitu ambacho hakipo" ameeleza mchungaji Boaz

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Zahanati Mashaka Nkonyoka amesema bado kanisa hilo lipo chini ya umiliki wa EAGT

"Lakini kimsingi kanisa hilo linaendeshwa na EAGT kama waanzilishi wa kanisa hilo siku zote ipo hivyo sasa imetokea kama wiki moja iliyopita mchungaji wa kanisa hilo Boazi Kazeba kubadilisha jina la kanisa hilo kutoka EAGT  na kuwa AGGCIA yani kanisa jipya"

Hadi EATV inatoka katika eneo hilo bado kanisa hilo lilikuwa limefungwa huku viongozi wa pande zote mbili wakipelekwa polisi kwa ajili ya mahojiano ili kutafuta suluhu ya mgogoro huo
 

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea