Thursday , 8th Dec , 2022

Uongozi wa Klabu ya Yanga umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa Yanga Princess Edna Lema na Kocha Msaidizi, Mohammed Hussein leo Disemba 8, kutokana na matokeo mabaya waliyoyapata kwenye mchezo wao dhidi ya Fountain Gate Princess kwa kupoteza 1-0.

Aidha Klabu ya Yanga  inawashukuru na kuwatakia kila la heri katika majukumu yao mengine huku wakidai hivi karibuni watangaza mbadala wa nafasi hizo hivi karibu.

ikumbukwe kuwa kocha huyo ambaye aliewezesha  timu hiyo ya Yanga Princess kumaliza katika nafasi ya pili katika ligi ya wanawake wakati kombe likichukuliwa tena na watani wao Simba.