
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema binti huyo alipigwa na radi hiyo na kufa papo hapo sambamba na mbuzi aliokuwa akiwafunga
Baba wa binti huyo pamoja na dada yake wameelezea masikitiko yao na kudai kuwa binti huyo alirejea nyumbani wiki moja iliyopita akitokea shuleni Mafinga mkoani Iringa kwa ajili ya likizo baada ya shule kufungwa