
Kamanda Maigwa akizungumza na #EATV amewataka wazazi kuwa waangalifu wanapotoka na watoto hasa katika maeneo yenye vilevi na mchanganyiko wa watu kwani sio salama kwa watoto hao
Ameeleza kuwa Jeshi la Polisi Kilimanjaro limejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa mkoa huo unakuwa na ulinzi wa kutosha katika kipindi hiki huku akitoa onyo kali kwa madereva wazembe na wanaotumia vilevi kuacha tabia hiyo kwani husababisha ajali zinazoepukika
Unaweza kusikiliza mahojiano yote kwenye video hii..