Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais Samia na kwamba anafuatilia hali ya Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.
Kwa upande wake mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mama Regina Lowassa, aamemshukuru Rais Samia kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia, huku mtoto wake Fredy Lowassa akiwashukuru Watanzania kwa maombi yao.