Tuesday , 3rd Jan , 2023

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kisarawe Selemen Jafo amewahakikishia wananchi kuwa serikali kupitia wizara ya mifugo imepanga kuchimba mabwawa na malambo maalum yatakayotumiwa na wafugaji kunyweshea mifugo yao

Lengo ni kupunguza muingiliano uliopo kati ya jamii za wakulima na wafugaji ambazo kwa kipindi kirefu zimekua katika migogoro na mapigano mara mara katika maeneo mengi nchini

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa semina ya kuwajengea uwezo viongozi wapya wa chama cha mapinduzi CCM wilayani Kisarawe waziri JAFO amesema uchimbaji wa malambo mbali na makazi ya wananchi na maeneo ya mashambani yatasaidia wakulima kuendesha shughuli zao kilimo bila kuingiliana na wafuagaji ambao wamekua wakipitisha mifugo katika mashamba kwa kisingizio cha kutafuta malisho na maji kwaajili ya mifugo yao kitu ambacho kimekua kikiibua mapigano ya mara kwa mara.

Awali wakulima kutoka maeneo mbalimbali wilayani Kisarawe wamesema kwa kipindi kirefu wamekuwa katika mgogoro kati yao na wafugaji ambao umekua ukikwamisha kufanya shughuli zao za kilimo kutokana na wafugaji jamii ya wamang'ati na wamaasai kupitisha mifugo yao kwenye mashamba kwa lazima na hata wanapoulizwa hujibu kwa jeuri huku wajitapa kuwa hakuna wakuwazuia kufanya hivyo