Friday , 13th Jan , 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki Sherehe za mwaka Mpya 2023 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 13 Januari, 2023

Katika hotuba yake mbele ya mabalozi hao Dkt. Samia ametoa wito kwa ofisi za balozi zinazowakilisha nchi zao  kuungana na Serikali kuhamisha ofisi zao kwenda Makao Makuu jijini Dodoma

“Mnafahamu kwamba Dodoma ndiyo makao makuu rasmi ya nchi yetu na Serikali imehamia huko na tunachukua kila hatua kuhakikisha linakuwa Jiji la kisasa na huduma zote muhimu.

“Tunapofanya hivyo tunawaomba mfanye mipango ya kuhamia pia kwenda kwenye makao makuu ya nchi yetu ili kunufaika na misaada mbalimbali ambayo Serikali inatoa kabla ya kumaliza wakati wake,” amesema Rais Samia katika hotuba yake

Amezitaka zifanye mawasiliano na mamlaka husika kupewa taarifa ya fursa zinazopatikana katika Jiji hilo