
Profesa George Wajackoyah
Wajackoyah ametoa ombi hilo akitaka maafisa hao wa polisi waruhusiwe kuvaa hijab chini ya kofia zao ili kuendana na imani yao ya Kiislamu hata wakiwa kazini.
"Ninataka wanawake wa Kiislamu ambao wapo kwenye vikosi vya polisi na jeshi wavae ile nguo yao ya Kiislamu inayofunika kichwa, (Hijab) tunataka Uislamu uonekane kila mahali nchini Kenya," amesema Profesa Wajackoyah
Aidha Profesa Wajackoyah pia ametoa rai kwa serikali kuwatengea mapumziko ya kila wiki waumini hao ili wapate muda wa kuabudu.