Wednesday , 18th Jan , 2023

Watu 18 wamepoteza maisha, akiwemo waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine, baada ya helikopta kuanguka kando ya shule ya chekechea katika kitongoji cha mashariki mwa mji mkuu Kyiv.

Helikopta hiyo inasemekana kugonga jengo la shule ya watoto kabla ya kuanguka.

 

Watoto watatu ni miongoni mwa waliofariki na wengine 15 wanatibiwa hospitalini. Waziri Denys Monastyrsky, alikuwa na wengine wanane kwenye helikopta hiyo.

Naibu waziri wake wa kwanza na waziri wa mambo ya nje pia walifariki, maafisa walisema, wakati helikopta hiyo iliposhuka katika kitongoji cha Brovary.