Wednesday , 18th Jan , 2023

Jeshi la Polisi nchini kupitia Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo limewataka wafanyabiashara wanaouza nyama kuhakikisha wanauza nyama ambazo zimegongwa mihuri toka mamlaka zinazohusika.

Kamanda wa kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua, akikagua nyama mkoani Arusha

Hayo yamesemwa hii leo Januari 18, 2022, na Kamanda wa kikosi hicho Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua, wakati alipotembelea mabucha ya kuuza nyama katika soko kuu la Arusha.

ACP Pasua amewataka wauza nyama wote kuhakikisha wanafuata kanuni na taratibu zinazowaongoza sambamba na kuuza nyama ambazo zinatoka katika machinjio ya serikali ambapo mifugo inapimwa kabla ya kuchinjwa.

Naye mkuu wa soko hilo Datus Renatus, mbali na kupongeza Jeshi la Polisi, amesema wamejifunza mambo mengi kupitia maelekezo mbalimbali ambayo wameyapata kutoka Polisi ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara wa nyama kuhakikisha wanafuata kanuni na taratibu za biashara zao.

Mwenyekiti wa mabucha  katika soko kuu la Arusha, Ezekiel Michael, amesema wamepokea changamoto ambazo wameambiwa na kuhaidi kuzifanyia kazi lakini pia akawataka wafanyabiasha wa nyama kucha tabia ya kununua mifugo ya wizi badala yake wanunue ile ambayo imefuata taratibu.