
Hayati Badara Alieu Joof
Makamu huyo wa rais alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi, ingawa Bw Barrow hakutaja ikiwa alikuwa akipokea matibabu nchini India.
Bw Joof hakuonekana hadharani kwa miezi kadhaa, ikiwa ni baada ya kuchaguliwa na Rais Barrow kama makamu wa rais baada ya kuchaguliwa tena mnamo Desemba 2021 kwa muhula wa pili.
Mwezi Juni, Bw Joof alielezea kutoridhishwa na mwenendo wa masuala ya umma, akisema Raia wa Gambia walikuwa na matarajio makubwa na mwendelezo wa mambo yale yale kiutendaji haitasababisha mabadiliko makubwa.