Rais Teodoro Obiang Nguema alitwaa madaraka 1979
Vyombo vya habari vya serikali vimesema Ruslan Obiang Nsue anadaiwa kuuza turboprop yenye siti 74 kwa kampuni iliyoko katika visiwa vya Canary.
Uchunguzi ulianzishwa mwaka jana ilipogundulika kuwa ndege hiyo ilikuwa imepotea wakati ikifanyiwa matengenezo ya kawaida nchini Uhispania.RPU
Mshukiwa huyo alikuwa akiendesha shirika la ndege la taifa nchini Equatorial Guinea, nchi ambayo iko imara mikononi mwa familia ya Rais Obiang Nguema ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 43.

