Wednesday , 1st Feb , 2023

Mamlaka ya uchaguzi nchini Nigeria ina wasiwasi kwamba uhaba unaoendelea wa mafuta nchini humo huenda ukaathiri maandalizi ya uchaguzi wa nchi hiyo utakaofanyika Februari 25.

Misururu ya usiku kucha imekuwa ikionekana katika vituo vya mafuta katika jiji kubwa zaidi nchini Nigeria, Lagos, kwani wengi hutumia saa nyingi kwenye mstari wakitarajia kununua mafuta.

Mamilioni nchini Nigeria wanategemea petroli, sio tu kwa usafiri, lakini kwa jenereta kwa ajili ya umeme  kwenye nyumba zao na biashara zao.

Gharama hizi zimepanda katika miezi michache iliyopita, huku bei ya mafuta ikipanda karibu 100% katika soko .

Serikali imekanusha kuongeza bei ya petroli na kushikilia msimamo  kuwa kuna usambazaji wa kutosha kukidhi mahitaji ya mafuta nchini humo.

Lakini inawalaumu wauzaji huru wa mafuta, ambao wana jukumu la kuuza na kusambaza bidhaa hiyo, kwa kuzidisha mzozo huo.