Monday , 6th Feb , 2023

Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga limekamata Lita 910 za mafuta ya dizeli yaliyokuwa yakitumika kwenye ujenzi wa reli ya kisasa SGR, katika msako wa polisi wamekamata pia mipira iliyokuwa ikitumika kufyonza mafuta hayo na kwenda kuuza kwenye migodi kwa wachimbaji

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amesema katika msako huo   pia wamekamata watuhumiwa tisa wa ujambazi  ambao wanadaiwa kuhusika katika tukio la kuvamia kambi ya raia wa kichina wanaojenga reli ya SGR eneo la Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni pamoja na kukamata bunduki moja kwenye kambi hiyo aina ya Shortgun Pump  action

Aidha pia walikamata fedha za nchi mbalimbali ikiwemo Naira 16,000 za Nigeria, Doĺlar 100500 za Vietnam, Yuan 20 za kichina  Dinar 1.5 za Kuwait na Rial 900 za Combodia ambazo ziliporwa na majambazi na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani.