Tuesday , 30th May , 2023

Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) kimeendelea kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa Maofisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali katika kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea.

Mkuu wa chuo cha DPA SACP lazaro Mambosasa, akizungumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari

Akitoa taarifa hiyo leo Mei 30,20223 Mkuu wa chuo hicho SACP Dkt. Lazaro Mambosasa, amesema kuwa chuo hicho kimekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa kozi mbalimbali wawapo chuoni hapo.

Ameendelea kueleza kuwa lengo la kutoa elimu hiyo ni kujenga uwezo kwa maofisa,wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa jeshi hilo na makundi mengine ya wahitaji ambapo amebainisha kuwa ni vyema kila askari kuwa na vifaa wezeshi ili kukabiliana na majanga hayo pindi yanapotokea.

Kwa upande wake Sajenti Saidi Hamad aliyepata janga la kuunguliwa moto nyumba yake ameushukuru uongozi wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kwa namna walivyoguswa na tukio hilo, ameongeza kuwa nyumba yake iliyopo Zanzibar iliteketea yote kwa moto ambapo anamshukuru Mungu familia imebaki salama.