Wednesday , 4th Mar , 2015

Pambano la Raundi 10 litakalomkutanisha Bondia Thomas Mashali na Dulla Mbabe linatarajia kufanyika Machi 15 mwaka huu, Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi Tanzania PST, Antony Rutta amesema, Pambano hilo litatanguliwa na Bondia Mada Maugo akipambana na Kalama Nyilawila huku japhet Kaseba akipanda kupambana na Said Mbelwa.

Rulla amesema, mapambano hayo yatasaidia mabondia hao kuweza kufanya vizuri katika mapambano mengine makubwa yaliyombele yao.