
Akizungumza mbele ya Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma. Wakili upande wa ulalamikaji Peter Madeleka amesema octoba 7 wali iomba mahakama iweze kutoa amri Fatma Kigondo kukamatwa kwa kutokufika mahakamani bila maelezo ya msingi kama alivyo amriwa agosti 23 kufika mahakamani pale ambapo kesi itakapotajwa ikitafsiriwa kama kudharau amri halali ya mahakama.
“Tarehe 23 agosti Mahakama ilitoa amri ya kwamba Fatma Kigondo afike mahakamani pale ambapo kesi yake itakuwa ikiitwa lakini tarehe 7 octoba 2024 hakufika Mahakamani na maana hiyo alikuwa amedharau amri halali ya mahakama na mahakama ikishatoa amri haiweze tena kwenda kinyume na Amri aliyoitoa yenyewe.” Amesema Wakili Peter Madeleka
Sambamba na hilo wakili madeleka amesema katika maamuzi ambayo yanasubiriwa kutolewa na mahakama ni pamoja na kunyimwa dhamana kwa Afande pindi atakapo kamwatwa kwani kesi inayomkabili ina hatarisha usalama wake. Na wamefika mahakamani tayari kusikiliza hukumu ya mahakama.