Polisi waeleza sababu ya watuhumiwa kutamba mtaani
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo, amewataka wananchi kujitokeza mahakamani kutoa ushahidi ili kuepukana na changamoto ya kesi nyingi kuharibika kutokana na ushahidi kukosekana, kitendo ambacho kinapelekea watuhumiwa wanaokamatwa kuendelea kutamba mtaani.

