Pele wa Brazil amewahi kuitembelea Yanga ?
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga wamethibitisha kuwa waliwahi kupata nafasi ya kutembelewa na klabu ya Santos ya Brazil pamoja na mfalme wa soka duniani Pele, japo ziara hiyo haikukamilika.