Chama: 
ADC
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Shoka Khamis Juma
Idadi Ya kura: 
0

Wilson Elias Mulumbe amezaliwa August 31, 1984 Handeni, Tanga

Wazazi wake walikuwa watumishi wa umma

Alipomaliza sekondari 2002 alianza ujasiriamali wa kusafirisha samaki kutoka Tanga kwenda Arusha

2011 alisoma stashahada ya sheria

Aliishi na kufanya biashara nchi za Botswana, Zimbabwe na Lesotho.

Amefunga ndoa na Grace Jackson na wana watoto wawili wote wa kiume.

2015 alijiunga na ACT WAZALENDO na alitangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Tanga kwa tiketi ya chama hicho kabla ya kuamua kuacha na kumuunga mkono rafiki yake mhandisi John Mapuri

Baadae akajiunga na CCM

2024 alijiunga na TLP kwa lengo la kuwania Urais aliposhindwa Julai 27,2025 akaibukia ADC