Georges Gabriel Bussungu ni mwanasiasa anayeamini katika mabadiliko ya fikra
Amezaliwa Aprili 23,1957 Kituo cha afya Makongoro Nyamagana Mwanza
Mama yake anaitwa Modesta Manungwa Nabeji na Baba yake ni Gabriel Fella Bussungu
Februari 05,1967 akiwa na miaka 9 alishiriki matembezi kuunga mkono azimio la Arusha
1969 alijiunga na vijana TANU na kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa vijana wa tawi
1970 akawa mwenyekiti wa TANU wilaya ya Nzega
Alikuwa na ndoto ya kuwa Kasisi wa Kanisa Katoliki
Amewahi kufanya kazi wizara ya viwanda na biashara akiwa Afisa biashara
Alijiunga na JKT na pia alishiriki vita vya Kagera
Ana stashahada ya uongozi,utawala, uhasibu alizozipata mwaka 1979,1986,
Pia ana shahada ya uongozi wa biashara aliyoipata mwaka 1990 chuo kikuu Mzumbe
Amewahi kuwa Katibu Tawala wa Mikoa ya Singida, Manyara kabla ya kustaafu kisheria mwaka 2017
Amekuwa mwanachama wa CCM tangu akiwa mtoto hadi mwaka 2021 alipojiunga rasmi ADA TADEA
Mwaka 2022 alichaguliwa na chama chake kuwa Naibu Katibu Mkuu
Mume wa Yasinta Medard Chuleha na Baba wa watoto kumi



















