Coaster Jimmy Kibonde amezaliwa Julai Mosi 1978 kwenye hospitali ya Meta jijini Mbeya
Mtoto wa Mama Hilda Mwanyasi Mwakajumba na Baba Jimmy Kibonde Mwakalobo ambaye kwa sasa ni Marehemu
Amewahi kuwa dereva bodaboda
Ndiye Mwenyekiti wa Chama Cha Makini
Alianza siasa akiwa kijana wa umri wa miaka 17 tu.
Mwaka 1995 alijiunga na Chama cha NCCR Mageuzi Mbeya kabla ya kuhamia chama cha MAKINI
Aliwahi kuwa mwenezi wa chama cha MAKINI
Pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa chama cha MAKINI
Kibonde amesaidia kubadilisha jina la chama cha MAKINI ambacho zamani kilikuwa kinajulikana kwa jina la Demokrasia MAKINI



















