Jumanne , 20th Nov , 2018

Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga amesema kuwa taasisi hiyo imeanzisha operesheni maalum ya ukaguzi na udhibiti wa uendeshaji biashara ya fedha jijini Arusha, na hii ni baada ya ukimya tangu jana baada ya kutokea sintofahamu katika biashara ya maduka ya kubadilishia

Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga.

fedha jijini humo.

Amesema hayo leo katika mkutano na wanahabari kufuatia tukio la askari polisi waliovalia sare za kijeshi kuonekana wakilinda maduka ya kubadilishia fedha jijini Arusha tangu jana asubuhi.

Uchunguzi wa Benki Kuu umebaini kuongezeka biashara ya ubadilishaji na utakatishaji fedha. Kuna maduka hayajasajiliwa lakini yanafanya biashara hii kinyume cha utaratibu,” amesema Profesa Luoga.

Profesa Luoga amesema wafanyabiashara ambao leseni zao zina makosa wanatakiwa kuzirejesha Benki Kuu kwani tayari zimefutwa na wanaoendesha maduka bila leseni kuacha mara moja.

Wote watakaobainika kukiuka sheria watafikishwa kwenye vyombo vya sheria na wote waliokuwa wanaendesha maduka hayo bila kufuata utaratibu leseni zao zimesitishwa", ameongeza Profesa Luoga.

Operesheni hiyo ni ya tatu kufanyika ikiratibiwa na kitengo cha uchunguzi cha benki hiyo, ambapo uchunguzi huo unafanywa kipindi ambacho BoT imesitisha maombi ya kuanzisha maduka mapya ya kubadilisha fedha.