Alhamisi , 22nd Dec , 2022

Wakati Mkoa wa Kagera ukitajwa kuwa miongoni mwa mikoa ya mwisho katika umaskini, maafisa kilimo wametakiwa kukaa na kupanga ni kilimo cha mazao gani kitaleta matokeo ya haraka ya kiuchumi kwa wananchi hasa vijana, lengo likiwa ni kuhakikisha uchumi wa mkoa unapanda kupitia sekta hiyo

Akizungumza katika kikao cha kamati ya kujadili maendeleo ya wilaya ya Bukoba, ambacho kimezishirikisha halmashauri mbili ambazo ni manispaa ya Bukoba na halmashauri ya wilaya ya Bukoba, mkurugenzi wa manispaa hiyo Hamed Njovu amesema kuwa, huwezi kuhamasisha kilimo cha miti au mazao ambayo yanaleta matokeo ya kiuchumi baada ya miaka 10 au 15, halafu ukategemea vijana waitikie.

"Vijana wanaangalia wafanye kitu gani cha kuwaletea matokeo ya haraka, na ndiyo maana wanakimbilia kwenye kuendesha bajaj na bodaboda, lakini maafisa kilimo wetu wakichagua zao ambalo linaweza likampa mkulima matokeo ya haraka, vijana wataenda huko" amesema.