Ijumaa , 23rd Dec , 2022

Jeshi la Polisi Nchini Kupitia Kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya (Anti Drug Unit), limesema kuwa jumla ya watuhumiwa 377 walitiwa hatiani kwa makosa ya kujihusisha na madawa ya kulevya na watu 170 walifungwa vifungo mbalimbali kwa makosa hayo.

Mkuu wa Polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya nchini ACP Amon Kakwale

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya nchini ACP Amon Kakwale.

ACP Kakwale amesema watu hao walikamatwa kwa kushirikiana na Polisi mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani na kusema kuwa kuanzia mwezi Julai hadi Novemba, 2022, jumla ya kesi 369 zilifikishwa mahakani na kutolewa uamuzi.

ACP Kakwale amekongeza kuwa vyombo vya moto vilivyo kamatwa na kutaifishwa ni magari 8, pikipiki 9, boti 02 na nyumba 01 vilitaifishwa na Mahakama kuwa mali za serikali.