Jumatano , 23rd Nov , 2022

 Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini TAWA imewajengea uwezo askari zaidi ya 20 kwa ajili ya kupambana na kukomesha uhalifu na uharamia wa majini unaofanywa na watu wasio waaminifu

Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku 30 katika chuo cha polisi wanamaji jijini Mwanza ambapo baadhi ya askari hao wamesema wapo tayari muda wowote kuanzia sasa kupambana na maharamia hao wanaofanya vitendo vya uhalifu ndani ya maziwa, mito na bahari

"Mfano mzuri kama mimi nilikuwa siwezi kabisa kuogolea nimefundishwa kuogolea na kuendesha chombo lakini pia kujiokoa na kuokoa wenzangu na ndani ya hifadhi kuna maeneo amabyo yana maji na kuna uhalifu mkubwa sana hii fura tuliyopata ya mafunzo itatusaidia kupambana na wahalifu hao"

Said Kabanda ni kamishna msaidizi wa usimamizi wa uhifadhi wa wanayamapori Tanzania TAWA ofisi ya kanda ya ziwa amesema mafunzo hayo yataleta tija kwa askari hao kupambana na wahalifu majini huku kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Mairi Makori akisema wamejipanga kikamilifu kukabiliana na wahalifu sehemu yoyote

"Lakini tumekuwa na changamoto ababu watu wetu walikuwa hawajapata mafunzo sahihi ya namna ya kukabiliana na uhalifu maeneo ya majini hadi hivi juzi tulipoteza askari wetu kwa kutokujua kuogelea"

"Maadui wanaweza wakatumia mito, maziwa kwa ajili ya kufanya uhalifu kwenye hifadhi sasa sisi kama askari ni jukumu letu ni kulinda hifadhi zetu na kupambana na majangili na wahalifu wote lazima tujue namna ya kujiokoa na kuwaokoa wengine"