Alhamisi , 8th Dec , 2022

Martin Kinasa mkazi wa mtaa wa Dkt Mohamed Shein, Kata ya Igoma jijini Mwanza, ameuawa kwa kupigwa kisha kuchomwa moto wakati akijaribu kuwatoroka watu waliokuwa wakimkimbiza kwa kutumia bodaboda kwa tuhuma za kwamba anasafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi.

Martin Kinasa aliyeuawa

Baadhi ya ndugu wa marehemu akiwemo Peter Kinasa wakizungumza na EATV amesema kuwa, "Ndugu yetu aliuawa na bodaboda baada ya kupata idhini kutoka kwa polisi kuwa tukamatieni huyo mtu anayekuja huko ni mwizi wa pikipiki, kwahiyo hiyo hali ndio ilisababisha ndugu yetu akatoka duniani"

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa, akizungumza kwa sharti la kutopigwa picha, amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo lililotokea Desemba Mosi mwaka huu katika kijiji cha Nyagili, Kata ya Chabula wilayani Magu.