Ijumaa , 8th Jul , 2016

Makampuni yanayotoa huduma za simu za mkononi na mawasiliano yametakiwa kuboresha huduma zao mara kwa mara ili kuleta matokeo chanya yanayoendana na wakati na mahitaji katika sekta ya mawasiliano nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Domiciana Mukama ambaye ni mkuu wa Vodacom kanda maalum ya Dar es salaam kuwa, ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia ya kidigitali kwenye mawasiliano ni vyema makapuni hayo yakawa wabunifu kwenye huduma zao.

Domician Mukama amesema, ubunifu kwa wateja sio jambo la kuingiza kipato pekee bali pia liendane na huduma muhimu kwa wakati muafaka nakutolea mfano uwepo wa simu ambayo imeunganishwa na teknolojia ya mtandao wa haraka ya 4G ya Tecno Camon C 9 ambayo kwa sasa ndio inayoongoza duniani.

Aidha, Domician amesema watanzania wasichukulie Camon C9 kama suala la kibiashara bali watambue kuwa simu hiyo inalengo la kuleta mapinduzi ya kiteknolojia katika sekta ya mawasiliano kulingana na ubora wake.