Jumamosi , 31st Dec , 2022

Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA John Mnyika amesema chama hicho kitashiriki uchaguzi mkuu wa 2025 iwapo serikali itaridhia masharti yao ikiwemo kuwaruhusu kufanya Mikutano ya hadhara katika mwaka 2023

Akizungumza wakati wa Kikao maalumu cha Chama hicho kilichohusisha majimbo ya Nyamagana na Ilemela, Mnyika amesema serikali lazima itekeleze masharti ya chama hicho kwa mwaka 2023 ikiwemo kuwasilisha muswada wa mabadiliko ya Katiba katika Bunge la Februari na kuwaruhusu kufanya mikutano ya hadhara kwani ni haki yao ya kisheria.

Kwa upande wake Mjumbe wa Balaza kuu CHADEMA John Heche amesema pamoja na mazungumzo baina ya chama hicho na serikali kuendelea bado hawaridhishwi na hali ya uchumi wa watanzania kulinganisha na rasilimali zilizopo