Jumapili , 19th Dec , 2021

Wizara ya afya imesema wanatarajia kuzindua kampeni nyingine ya Kinga ya UVIKO-19 Uzinduzi utakaofanyika Jijini Arusha Desemba 22 mwaka huu.

Katibu Mkuu Wizara wa Afya Prof. Abeli Makubi

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara wa Afya Prof. Abeli Makubi, amesema kuwa katika Kampeni  hiyo wizara itashirikiana na Wizara ya TAMISEMI lengo likiwa ni kuwafikia wananchi kwenye mitaa yao, vitongoji pamoja vijiji vyao

Prof. Makubi amesema kampeni hiyo itawashirikisha wasanii mbalimbali,viongozi wa Kijiji na vikundi mbalimbali vya kimila ili kuwezesha kuwafikia wananchi kwa urahisi

Aidha Prof. Makubi amesema kuwa mpaka sasa watu waliopatiwa chanjo ya UVIKO-19 ni asilimia 2.2 huku malengo ni kufikia asilimia 60.