Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo
Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 21, 2021, na Kamanda wa Polisi mkoani humo Justine Masejo, ambapo amesema kuwa tukio hilo limetokea Juni 19, 2021, majira ya saa 12:00 jioni, na binti huyo ameajiriwa miezi miwili iliyopita akitokea mkoani Mara.
Aidha, ACP Masejo ameongeza kuwa wanaendelea kumshikilia binti huyo ili kujua nini kilipelekea kuchukua maamuzi hayo na kwamba upelelezi utakapokamilika jarida lake litapelekwa Ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa uamuzi wa kisheria.


