
Adha ya usafiri eneo la Jangwani wakati wa mvua.
Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 16, 2020, hii ni kufuatia uwepo wa mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo, iliyopelekea eneo la Jangwani kujaa maji na hivyo barabara hiyo kutopitika.
"Tunawashauri wasafiri wa mabasi ya Mwendokasi wanaotokea Kimara kuelekea mjini-kati kuwa watumie mabasi hayo mpaka Morocco, halafu wachukue usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka mjini-kati, Kariakoo na sehemu nyingine za jiji. Hivyo hivyo, wale wanaotokea mjini-kati kwenda Kimara, wachukue usafiri mbadala mpaka Morocco ambapo wanaweza kuendelea na usafiri wa mabasi ya Mwendokasi kuelekea Kimara" imeeleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imeeleza kuwa mvua iliyonyesha leo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara, itaendelea kunyesha hadi kesho Januari 17, 2020.