Jumatatu , 15th Jan , 2018

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Flava Dudubaya ameamua kuachana na matumizi ya  pombe na kuamua kumrudia Mungu ili kuufanya mwaka 2018 uwe wa mafanikio kwake.

Dudu Baya amekiri kuwa Pombe ilimfaya akashidwa kuzuia hasira zake ikiwa ni pamoja na kushidwa kufanya ibada.

Ujumbe alioutuma Mamba Dudubaya kwenye barua pepe ya Producer wa Planet Bongo Dudubaya amesema kwamba mwezi 5 2017 alichoka maisha ya pombe na ndiyo maana akarudi mbele za Mungu ili kumshirikisha Mungu kuhusu kuacha pombe na hatimaye amefanikiwa kuingia mwaka 2018 akiwa msafi kabisa.

"Si rahisi kumuacha shetani wa pombe kama mtu hajakushirikisha wewe Mwenyezi Mungu. Huwezi kumuokoa mtua ambaye hayupo tayari kuokolowa. Mwaka 2017 umeniokoa. New Person, New Life. Nauanza mwaka 2018 nikiwa Mamba Dudubaya, Oil Chafu Konki Masta. ..So Fresh ..So Clean," Sehemu ya maombi ya Dudubaya.

Msikilize hapa chini