
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola.
Kangi Lugola ametoa kauli hiyo akiwa Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na www.eatv.tv iliyotaka kufahamu juu ya mkanganyiko uliojitokeza kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonakana baadhi ya Makamanda wakiendelea kufanya kazi kwenye vyeo vyao.
Kangi Lugola amesema "sina taarifa kwamba agizo langu halijatekelezwa lakini kwa sababu nilimpa muda wa utekelezaji IGP kwa hiyo naamini litatekelezwa, saa nyingine watu hawajui kutengua mtu ni mamlaka na mimi ndiye nina mamlaka."
"Utekelezaji ndiyo unaendelea sidhani kama wamekaidi au IGP amekaidi kutekeleza agizo langu." ameongeza Kangi Lugola.
Juzi Kangi Lugola alitoa uamuzi huo wa kutengua uteuzi wa makamanda wa polisi wa mikoa mitatu akiwemo Salum Hamduni aliyekuwa Ilala, Emmanuel Lukula (Temeke) kwa kosa la kushindwa kusimamia mianya ya rushwa na utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa.