Alhamisi , 6th Oct , 2022

Kundi la 12 la waliokuwa wakazi wa Ngorongoro limeomeondoka leo kuelekiea kijiji cha Msomera mkoani Tanga kupisha shughuli za uhifadhi katika hifadhi ya Ngorongoro. Kundi hilo linajumuisha kaya 61 zenye watu 310 na mifugo 2000

Wakizungumzia kuondoka kwao baadhi ya watu mashuhuri wakiwemo viongozi wa dini wamesema wanatumaini jipya katika mwendelezo wa shughuli pindi watakapo fika kijiji cha Msomera 

Akiliaga kundi hilo Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Raymond Mangwala amesema kutokana na hamasa ya kuondoa kwa hiari imewalazimu kuanza kufikiria utaratibu mwingine ili waendane na kasi hiyo ikiwemo kuongeza waandikishaji na kasi ya ujenzi wa nyumba zaidi Msomera