Idadi hiyo inafanya jumla ya wakazi wa Ngorongoro ambao tayari wameshahamia Msomera mpaka sasa kuwa watu 2629 na mifugo 14132
Kundi hili ambalo ni la kwanza kuondoka ngorongoro Kuelekea Msomera kwa mwaka huu limejumuisha watu maarufu katika jamii wakiwemo viongozi wa mila wa jamii ya Kimaasai naarufu kama Malaigwanani pamoja na vijana ambao kwa pamoja wameonekana kuwa na tumaini jipya la Maisha yao
Akiwaaga wakazi hao Mkuu wa Wilaya ya ngorongoro Mwalimu Raymond Mangwala amewahakikishia wakazi hao huduma bora za kijamii ukilinganisha na zile walizo kuwa wakipata Ngorongoro


