Machinga
Wamesema maeneo ya mjini wanayohitaji kupangwa ni pamoja na Makoroboi, Sahara pamoja na eneo la Dampo, ambayo tangu zoezi la kuwapanga lilipoanza waliyaomba leo hii wameamua kupaza sauti zao na kuomba huruma ili waweze kufanya shughuli zao kati kati ya jiji ambapo kuna wateja
"Watu wana njaa hakuna mtu anaweza kupigana kama hana njaa, watoto wanalala njaa, njaa ndiyo inayotusumbua na machinga kwa sasa ni watulivu sana hawana shida yoyote tulikaa tukasubiri kupewa majibu kama tunabaki Makoroboi au la lakini hadi leo kupo kimya ndiyo maana leo unaona mambo yamekuwa hivi," amesema mmoja wa machinga hao
Godfrey Malya ni mfanyabiashara mkubwa jijini Mwanza amesema kufuatia vurugu zilizotokea leo ameshindwa kufungua duka lake huku akiambulia kupigwa mawe
Akizungumzaa EATV kwa njia ya simu mwenyekiti wa machinga wilaya ya Nyamagana Matandura Ramadhan amesema.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limezima vurugu za machinga na mgambo kwa kuwatawanya na kuwakamata vijana wawili wanahojiwa kuhusu vurugu hizo.
"Hali ya usalama ipo vizuri wafanyabiashra wanaendelea na shughuli zao kama kawaida na kuendela kuwasaka vijana wengine waliohusika na vurugu hizo na kuwajulisha wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao kama kawaida kutokana na jeshi hilo kuimarisha ulinzi," Amesema RPC Mwanza Wilbroad Mutafungwa