Jumamosi , 15th Oct , 2022

Ofisi ya Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya Jinai kwa kushirikiana na taasisi nyingine za uchunguzi na za kifedha wameanza uchunguzi wa madai ya wananchi kutapeliwa na kampuni inayofahamika kama Kalynda E-Commerce Ltd huku wananchi wakitakiwa kuwa makini na matapeli wa mitandaoni

Msemaji wa  Jeshi la Polisi David Misime

Msemaji wa  Jeshi la Polisi David Misime amewataka wananchi kama wanataka kuwekeza kuhakikisha wanawekeza kwenye taasisi za kifedha zilizopo kwa mujibu wa sheria 

Aidha, Polisi wametoa rai pale mwananchi  atakapo baini kampuni  zenye mwenendo  wa aina hiyo wasisite kutoa taarifa  mapema iii hatua stahiki zichukuliwe.