Jumanne , 5th Dec , 2023

Mtu mmoja amefariki dunia huku kaya zaidi ya 200 zikikosa Makazi ya kuishi kufuatia mafuriko yaliyotokea usiku wa kuamkia tika kata  4 za Wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro

Nyumba kadhaa zimezingirwa na maji katika kiji cha Rudewa Batini Wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro baada ya moto wami kufurika

Mkuu wa Wilaya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amethibitisha madhara hayo

"Tulipata mvua za wastani jana majira saa 11 jioni ila tumepokea maji mengi kutoka milimani kupitia mto mkondoa na wami ambapo mto wami umepasua na maji kuingia mtaani nyumba zimeharibika na baadhi ya mali za wananchi katika kata Rudewa na Mvumi zaidi lakini tumepata kifo cha Mtu moja mtu mzima mwanume"

Aidha Shaka amesema tayari serikali imetenga maeneo ya kuwasaidia wahanga wa mvua hizo 

"Serikali imetenga maeneo maalum kwa ajili ya wahanga wa mafuriko na taratibu nyingine za kusaidia hudumu muhimu za kibinadamu, kwa upande wa kilosa sec ambako nako kumetokea uharibifu wa miundo mbinu ya vyoo nimelekeza wanafunzi ambao wamemaliza mitihani yao waruhusiwe kurudi majumbani nyakati hizi tukiendea na jitihada za kurudi miundo mbinu shuleni hapo" amesema Shaka Hamdu Shaka