Jumatatu , 28th Aug , 2017

Mahakama ya Juu nchini Kenya imekubali ombi la muungano wa vyama vya upinzani nchini humo Nasa, kukagua 'server' na mfumo mzima wa kompyuta zilizotumiwa na Tume ya Uchaguzi IEBC wakati wa uchaguzi mkuu uliyoyafanyika Agosti 8 mwaka huu.

Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya mmoja wa wagombea urais kupitia muungano huo Raila Odinga kuwasilisha kesi Mahakamani kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta wa kupitia chama cha Jubilee ambapo kwa sasa wataweza kupitia matokeo hayo lakini wakiwa chini ya uangalizi ili kuhakikisha usalama wa mitambo ya IEBC isihujumiwe.

Pamoja na hayo, wataweza kupata taarifa kuhusu yaliyojiri katika mitambo hiyo ya uchaguzi kuanzia Agosti 5 mpaka kufikia leo hii pamoja na kusoma nakala za Fomu 34A na 34B ambazo ni za matokeo ya vituo vilivyotumika kupiga kura kwa ngazi ya maeneo ambazo zilitumiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.