Malipo ya pensheni yapaa ndani ya miaka 2 Zanzibar

Jumapili , 12th Jan , 2020

Sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanyika leo katika Uwanja wa Amani, Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiongozwa na Rais Magufuli.

Rais Dkt. Ali Mohamed Shein

Mgeni rasmi katika sherehe hizo ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.

Katika hotuba yake kwa wananchi kwenye sherehe hizo, Dkt. Shein amesema kuwa Serikali ya Awamu ya 7 ndani ya miaka yake tisa imeendelea kutekeleza mipango ya mageuzi ya kiuchumi kwa kuimarisha hali ya amani iliyopelekea kuongezeka kwa pato la uchumi mara sita zaidi. Kutoka  Trilioni 1.78 mwaka 2010 Trilioni 2.87 mwaka 2018.

Pia amesema kuwa Pato la mwananchi limeongezeka kutoka wastani wa Sh. 942,000 mwaka 2010 hadi kufikia Sh. 2,323,000 mwaka 2018 jambo lililopelekea kuinua hali ya maisha ya wananchi.

Kuhusu ulipaji wa pensheni kwa wastaafu, amesema kuwa, "malipo ya pensheni kwa wastaafu yameongezeka kutoka Sh. 25,000 kwa mwezi mwaka 2017 hadi Sh 90,000 kwa mwezi mwaka 2019".