Jumamosi , 21st Mei , 2022

Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wa Chama hicho James Mbatia na Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Angelina Mtahiwa, na kuwataka kutojihusisha na shughuli zozote za chama, kutokana na tabia za kukosa uaminifu.

James Mbatia

Uamuzi huo umetolewa hii leo Mei 21, 2022, kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kugombanisha viongozi na kulazimisha kujiuzulu pamoja na tuhuma zingine.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mwenyekiti wa azimio hilo, Joseph Selasini amesema pamoja na kusimamishwa kwa viongozi hao pia wamelivunja Baraza la Wadhamini la NCCR  na kuteua wajumbe wapya ambao watasajiliwa kwa mujibu wa taratibu zitakazowekwa.