Mbunge wa CHADEMA aliyehamia CCM ajivunia Magufuli

Alhamisi , 25th Jun , 2020

Mbunge wa Viti Maalumu Anna Joram Gidarya ambaye amehama CHADEMA na kujiunga na CCM leo Juni 25, 2020 amefika katika ofisi za CCM Wilaya ya Babati mkoani Manyara na kuchukua kadi ya CCM pamoja na kula kiapo rasmi kuanza kukitumikia chama hicho.

Anna Joram Gidarya (wa pili kutoka kushoto)

Baada ya kula kiapo, Anna Gidarya amesema kwa kazi aliyofanya Rais Magufuli hata wapinzani hawana hoja tena maana tayari hoja zote zimeshafanyiwa kazi ndio maana yeye ameamua kurudi nyumbani.

''Nilikuwa kama napoteza taswira ya kisiasa na kujikuta nakuwa sio mzalendo wa nchi yangu naahidi kusema niliyokutana nayo kipindi kizima nilichokuwa upinzani'', amesema.

Tazama Video hapo chini