
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
Chongolo ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu kwa ufaulu mzuri wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 iliyofanyika katika viwanja vya Polisi Officers Mess.
Aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano imetoa elimu bure bila malipo na kwamba suala la kuchelewa kukamilisha mahitaji hayo isiwe sababu ya kuwazuia watoto hao wa wanyonge kushindwa kuanza masomo yao.
“ Kuna baadhi ya maeneo nimesikia kuna wakuu wa shule wanawarudisha nyumbani watoto kwa sababu hawajakamilisha mahitaji yao, kama mtoto hana viatu, sijui nini waache wasome wakati wazazi wao wanawatafutia mahitaji hayo, naomba nisikie mwanafunzi amerudishwa nyumbani kwenye wilaya yangu” amesisitiza Mhe. Chongolo.
Alisema ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ilianzisha mkakati wa ujenzi wa madarasa 100, ambapo kwa Shule ya Sekondari ni Madarasa 40 huku Shule ya Msingi Madarasa 60 lengo likiwa ni kuongeza tija katika taaluma.