Jumatano , 31st Mar , 2021

Ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mtangazaji wa ITV/Radio One Blandina Sembu, imefanyika leo Machi 31, 2021, katika kanisa Katoliki Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Mwili wa Blandina ukiwa Kanisani

Ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzake wa ITV/Radio One pamoja na wafanyakazi wengine wa makampuni wa IPP walishiriki Ibada hiyo na kutoa heshima zao za mwisho.

Baada ya ibada mwili wa marehemu Blandina ulianza safari ya kuelekea nyumbani kwao mkoani Mara kwa ajili ya maziko.

Waombolezaji wakiwa kanisani

Wakati wa uhai wake Marehemu Blandina alikuwa akiandaa na kutangaza kipindi Jarida la Wanawake, kinachorushwa na ITV.

Waombolezaji kwenye ibada ya kuaga mwili wa Blandina

Machi 28, 2021, mwili wake ulikutwa umetupwa njia panda ya ITV maeneo ya Mwenge Dar es Salaam na Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni kuthibitisha kuwa amefariki dunia.

Jeshi la Polisi limeeleza kwamba linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo la kuuawa mtangazaji huyo wa ITV Blandina Sembu.