Ijumaa , 20th Mei , 2022

Mwanamke aitwaye Mariam mkazi wa Sinza Lion Dar es Salaam, amejeruhiwa kwa kupigwa risasi maeneo ya begani katika harakati za Polisi kuwatuliza raia wenye hasira kali waliokuwa wanataka kumpiga mwizi aliyekwapua simu kwenye bodaboda majira ya saa 12:00 asubuhi ya leo Mei 20, 2022.

Sehemu ambayo tukio la mwanamke kujeruhiwa limetokea

Kwa maelezo ya mashuhuda wa tukio hilo, wanadai baada mwizi huyo kukwapua simu alikimbilia nyumba iliyokuwa jirani na baadaye kidogo walitokea maaskari waliomwokoa mwizi lakini katika harakati za kuwatuliza raia, inadaiwa walifyatua risasi iliyomjeruhi raia huyo ambaye amekimbizwa hospitali.