
Mwili wa Mama mzazi wa Erick Kabendera, ukiwasili Bukoba
Mwili wa mama mzazi wa mwandishi wa habari anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, Erick Kabendera, umewasili katika uwanja wa ndege wa mjini Bukoba na kupokelewa na ndugu na jamaa, ukitokea mkoa wa Dar-Es-Salaam.
Akizunguza wakati wa mapokezi ya mwili wa mama huyo Verdiana Mujwahuzi, baba mdogo wa Erick, Almachius Kabendera amesema kuwa, mwili huo utahifadhiwa kwa muda katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera, na baadae utapelekwa kijiji na kata Katoma Bukoba vijijini kwa ajili ya mazishi.
"Tumefika leo Asubuhi, tutaenda Rwamishenye ambapo pia kuna mji wa mama, lakini baadae tutaenda Katoma kwa ajili ya mazishi siku ya Jumatatu wiki ijayo" amesema Almachius.
Mama wa Erick Kabendera alifariki dunia siku ya Disemba 31, 2019, katika hospitali ya Amana iliyoko jijini Dar-Es-Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
#HABARI Mwili wa Mama mzazi wa Mwandishi wa Habari Erick Kabendera, umewasili katika Uwanja wa Ndege wa Mjini Bukoba na kupokelewa na ndugu na jamaa, ukitokea jijini Dar es salaam. pic.twitter.com/YUJTrB4wAy
— East Africa Radio (@earadiofm) January 4, 2020
Tazama mapokezi hapo chini.