
Hayati baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere
Nyumbani Kwa mwalimu Nyerere Magomeni Dar es Salaam Nyumba ya kwanza iliyotajwa kufanyia harakati mbalimbali za uhuru na hapa baadhi ya Wakazi wa Dar es Salaam wanamzungumza mwalimu kama mhifadhi namba Moja katika maliasili za nchi ikiwemo hifadhi,madini pamoja na Mali kale.
Pamoja na hivyo bado serikali imekuwa ikifanya mikakati mbalimbali ili kuhakikisha vijana wa leo wanafahamu nini ilikuwa chimbuko la Mwalimu Nyerere Kupenda kukutana katika michezo mbalimbali ili kuimarisha hali ya kisiasa kipindi kile cha ukoloni.
Hata hivyo wazee hao wamewataka vijana wa sasa waliopata nafasi ya masomo kuzitunza falsafa na maadili aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere Enzi za utawala wake.